InterNICHE



  About InterNICHE
  News
  Alternatives
  Conscientious Objection
  Resources
  How you can help
  Sponsors
  Site Map
  Links
  HOME

Introduction in other languages


 



InterNICHE Co-ordinator
Nick Jukes
42 South Knighton Road 
Leicester LE2 3LP 
England 

Tel/Fax +44 116 2109652

coordinator@interniche.org



 Introduction - Kiswahili

 

Unafikiri utumizi wa wanyama katika majaribio hukufunza nini?

 

Hakuna sababu ya wanyama kuuliwa ili kupasuliwa na kutumika katika majaribio ya kielimu na mafunzo. Mbinu mpya na za kisasa zisizowadhuru wanyama zipo kwa wingi na zimekuwa zikitumika kwa kawaida katika vyuo vikuu vingi.

 

Elimu ya kimaadili isiyo wadhuru wanyama inahusu utumiaji wa mbinu ambazo ni bora zaidi na pia zifaazo zaidi katika yale malengo ya kufunza.Teknolojia ya hali ya juu ya kompyuta inatoa uwezekano mwingi sana, kuanzia upasuaji wa wanyama mtandaoni, majaribio ya maabarani katika kioo, hadi uigaji kihalisia mtandaoni wa taratibu za kimatibabu. Nyenzo za mafunzo ya kisasa pia zinahusisha utumiaji wa wanyama bandia katika miundo midogo ya upasuaji yani ‘microsurgery” pamoja na vyumbe kama wanyama halisi vilivyo na viungo bandia na utaratibu wa mwitikio yani “feedback”. Mbinu nyingine zinahusu kichechemuo cha mishipa kutumia mitambo inayopitia kwa kompyuta kutokana na majaribio binafsi ya wanafunzi wa kujitolea.

 

Elimu ya kimaadili huweza pia kuwahusisha wanyama wenyewe.Wakati wanafunzi wa udaktari wa wanyama wanaposaidia wenzao walio na tajiriba katika utibabu, wakiwa na wagonjwa wa ukweli,wanajifunza mbinu za kimatibabu pana na zenye mseto kama vile utunzaji wa wagonjwa na heshima kwa maisha –kinyume na majaribio ya wanyama ambayo yanawafunza kwamba wanyama ni kama vyombo vya kutupa.Wakati wanafunzi wa biolojia wanasoma wanyama katika maeneo yao halisi ya kuishi, kwa kutumia mbinu zisizowadhuru wanyama hao,basi wanajifunza mengi zaidi kuhusu nyendo za wanyama kuliko vile majaribio ya wanyama katika maabara yangewafunza. Na kwa kuenda sambamba na upasuaji unaofanywa na wanafunzi wa udaktari wa wanadamu, kupitia miili ya wanadamu waliofariki,wanafunzi wa udaktari wa wanyama na wanafunzi wa biolojia vilevile wanaweza kufanya upasuaji wa kimaadili kupitia wanyama ambao wamekufa kwa ugonjwa au jeraha.

 

Matumizi ya wanyama waliouawa kwa majaribio hayatawafunza wanafunzi na wakufunzi zaidi kuhusu somo hilo kuliko vile ambavyo mbinu za kimaadili zingewafunza. Hata hivyo, majaribio ya wanyama yapo pekee katika kukulazimisha kuchukua mtazamo kuwa maisha ya mnyama si muhimu. Je, kweli tunawataka daktari wa wanyama,watafiti na daktari wote kwa ujumla ambao wamefunzwa kuwa viumbe hai vinaweza kutumiwa na kutupwa? Na je inafaa kuondoa wanyama kutoka maeneo yao halisia au kuwafungia kwenye vizimba vidogo vidogo maisha yao yote,wasiwahi kutekeleza matakwa ya maumbile yao na hatimaye kuishia katika sinia la upasuaji au kutayarishwa kwa majaribio maharibifu?

 

Masomo yaliyochapishwa yameonyesha kwamba maarifa, mbinu na utambuzi wa maadili unaweza kufahamika zaidi kwa kutumia mbinu zinazoendelea na tofauti. Badala ya kulazimishwa kuvunja imani zao za kimaadili,wanafunzi na wakufunzi wanaweza kuyafurahia mazingira bora zaidi ya mafunzo iwapo hawatatumia mbinu zinazoumiza wanyama.Wewe una uwezo na nguvu za kuleta mabadiliko.Wasiliana na InterNICHE kwa msaada ili kukomesha matumizi haribifu ya wanyama.Chagua elimu ya kimaadili.

News release
Other languages


 About InterNICHE
 News
 Resources
 Alternatives
 Conscientious
   Objection

 How you can help
 Sponsors
 Site Map
 Links
 HOME
o